Taasisi ya MVIWAARUSHA na washirika wa mradi wa KEA amabo ni IDP NA CARI wameandaa tuzo za waandishi wa habari kwenye mfumo endelevu wa chakula na kilimo Ikolojia zenye lengo la kutambua na kusherehekea uandishi wa habari uliotukuka kwenye masuala muhimu yanayohusiana na kilimo endelevu, usalama wa chakula na uendelevu wa mifumo ya chakula.
Tuzo hizo zitalenga kuhamasisha ubora katika uandishi wa habari ,kuhimiza ufuatiliaji wa kina kuhusu mbinu za kilimo cha kiikolojia na kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa mifumo endelevu ya chakula mbele ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi na ongezeko a idadi ya watu.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mapema mwezi Disemba mwaka 2024 na zitatolewa kwa waandishi wa habari kutoka maeneo mbali mbali nchi ambao walipatiwa mafunzo na Taasisi hiyo ya MVIWAARUSHA mwaka 2022.

Shares:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *